Kitengo cha Dini kimegawa maelfu ya machapisho kwa mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimegawa maelfu ya machapisho yenye mafundisho tofauti ya Dini, yanayo jenga maarifa kwa mazuwaru kuhusu ziara ya Arubaini.

Machapisho hayo yamegawiwa kupitia vituo vyake vilivyo funguliwa kwenye barabara zote zinazo elekea Karbala tukufu, vinavyo simamiwa na idadi kubwa ya masayyid na mashekhe wahudumu wa kitengo, sambamba na kuandika baadhi ya miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya kwenye machapisho hayo.

Tangu mwanzo kitengo kimekua kikitoa maelfu ya machapisho kuhusu ziara hii, machapisho yapo ya aina tofauti, kuna vitabu vidogovidogo, folda na vipeperushi, kuna yanayoelezea ziara na mambo ya kisheria na kijamii, aidha kuna mambo yanayohusu hijabu, swala na maadhimisho ya Husseiniyya, kwa kiasi cha kumjenga zaairu kidini na kiakili.

Kumbuka kuwa kitengo cha Dini kimeweka vituo sehemu nyingi za barabara zinazoelekea Karbala, vyenye jukumu la kujibu maswali ya mazuwaru, na kutoa maelekezo ya kifiqhi, kiaqida na kimaadili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: