Usomaji wa Qur’ani kwa ajili ya mashahidi wa fatwa tukufu ya kujilinda na wanajeshi wa serikali katika barabara ya (Yaa Hussein)

Maoni katika picha
Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya wa nje uliopo katika barabara ya Najafu, umetoa huduma mbalimbali, miongoni mwa huduma hizo ni usomaji wa Qur’ani kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwarehemu mashahidi wa fatwa tukufu ya kujilinda na wale wa jeshi la serikali, waliojitolea nafsi zao kwa ajili ya kulinda matembezi haya na taifa la Iraq na maeneo matakatifu.

Kwa mujibu wa msimamizi wa kituo cha usomaji huo wa Qur’ani Shekh Hussein Turabi amesema: “Tumegawa majuzuu ya Qur’ani tukufu, na tunatoa nafasi kwa zaairu kusoma juzuu analotaka, kwa lengo la kusoma Qur’ani mara nyingi zaidi na kuelekeza thawabu za kisomo hicho kwa mashahidi wa fatwa tukufu na wanajeshi wa serikali, hakika walitoa damu zao takatifu kwa ajili ya taifa hili, kwa utukufu wa damu zao zilizo mwagika matembezi haya yameweza kuendelea na raia wote wa Iraq wamepata neema ya amani”.

Akasisitiza kuwa: “Hili ni jambo dogo sana tunaloweza kuwafanyia, damu zao zilifanikiwa kumaliza njama za maadui, hakika roho zao ni taa liangazalo mbingu ya barabara hii na taifa hili, hii ni sehemu ya wajibu wetu kwao, kwa heshima kubwa na unyenyekevu tumeamua kufanya hivi”.

Akamaliza kwa kusema: “Jambo hili linafanywa kwa mwaka wa kwanza, na limepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru, tumekhitimisha mara nyingi na tunatarajia kuendelea na ratiba hii katika ziara zijazo, kumbukumbu zao zidumu kama yanavyodumu matembezi haya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: