Kikosi cha Abbasi kimetangaza kufanikiwa kwa mkakati wake wa kusimamia ulinzi na kutoa huduma

Maoni katika picha
Uongozi wa kikosi cha Abbasi cha wapiganaji umetangaza kufanikiwa kwa mkakati wake wa kusimamia ulinzi na kutoa huduma katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ya mwaka huu 1443 hujiriyya.

Kiongozi wa kikosi cha Abbasi cha wapiganaji Shekh Maitham Zaidi amesema: “Mikono yetu imepata utukufu wa kugusa zaisi ya mazuwaru milioni 10, wakati wa kutekeleza jukumu la ukaguzi, akasema kuwa kufanikiwa kwa kikosi kunatokana na baraka za Mwenyezi Mungu mtukufu na Mitume wake hususa wa mwisho wao Muhammad na Aali Baiti wake (a.s), na Marjaa Dini mkuu na waumini pamoja na raia wema wa Iraq”.

Akasisitiza kuwa: “Hashdu Atabaat tukufu itaendelea kuwa baba wa wote kwa kutumikia wananchi na mazuwaru watukufu”.

Akasema kuwa jukumu lijalo tutakuwa Najafu katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).

Akaendelea kusema: “Bendera ya Hashdu Atabaat imepandishwa katika ziara hii, tupo kusheria na kikatiba.. kisheria kwa sababu tunafungamana na Ataba tukufu, na kikatiba kwa sababu ya kufungamana na jeshi la serikali na kufanya kazi pamoja nao”.

Kiongozi wa kikosi cha Abbasi cha wapiganaji akatoa shukrani kwa Marjaa Dini mkuu na Atabatu Abbasiyya tukufu, akasema: kama sio kilemba kitukufu cha Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani isingeundwa Hashdu na lisingekombolewa taifa la Iraq na kupata utulivu uliopo.

Akaendelea kusema: “Sisi kama kikosi cha Abbasi cha wapiganaji tunatoa shukrani maalum kwa Atabatu Abbasiyya kupitia kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi pamoja na Mheshimiwa katibu mkuu na wajumbe wa kamati kuu bila kusahau vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake, kama sio watu hao watukufu kikosi cha Abbasi kisingekuwepo”.

Akasema: “Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji kimefunga huduma zake baada ya maukibu yake kushiriki kwenye ziara ya Arubaini na kuomboleza katika mji mtukufu wa Karbala mbele ya viongozi wa kikosi na wapiganaji wake pamoja na kundi kubwa la watumishi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: