Muhimu: Ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani yatoa tamko kuhusu uchaguzi ujao wa bunge hapa Iraq

Maoni katika picha
Ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani leo Jumatano (21 Safar 1443h) sawa na tarehe (29 Septemba 2021m), imetoa tamko muhimu kuhusu uchaguzi ujao wa bunge hapa Iraq, katika jibu la swali kutoka kwa kikundi cha waumini kuhusu uchaguzi huo, lifuatalo ni tamko hilo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Sistani

Amani ya Mwenyezi Mungu na baraka zake ziwe juu yenu

Msimu wa uchaguzi wa bunge la Iraq umekaribia, wananchi wengi wanauliza kuhusu msimamo wa Marjaa Dini mkuu kuhusu kushiriki kwenye uchaguzi huo, inaona kitu gani kinafaa katika hilo? Tunaomba ufafanuzi katika jambo hilo, shukran.

Kundi la wananchi

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Hakika Marjaa Dini mkuu anahimiza watu wote washiriki kwenye uchaguzi, Pamoja na kwamba hautasalimika na baadhi ya mapungufu, lakini itaendelea kuwa njia salama ya kuvusha taifa katika hali ya mbaya na kuelekea kwenye hali nzuri, aidha ni njia ya kuondoa taifa kwenye vurugu na mkwamo wa kisiasa.

Washiriki wanatakiwa kutumia uzowefu wa chaguzi zilizo pita na kuthamini kura zao kwani ni muhimu kwa mustakbali wa taifa, watumie nafasi hiyo muhimu katika kuleta mabadiliko ya kweli katika idara za serikali, kwa kuondoa mafisadi na watu wasiofaa, jambo hilo linawezekana pale watu wenye uwelewa watakapo jitokeza kwa wingi kupiga kura na wakachagua vizuri, wasipo fanya hivyo mambo yataendelea yaleyale ya zamani, Marjaa Dini mkuu anasisitiza tamko kama hili alilotoa karibu na uchaguzi uliopita, kuwa haungi mkono mgombea yeyote au mlengo fulani, uwanja uko wazi kwa wananchi waangalie yeyote anaewafaa.

Lakini anasisitiza wachunguze historia za wagombea na wala wasichague ispokua wanaeona anafaa, mwenye uchungu na taifa la Iraq, wajihadhari na kuchagua watu wasiofaa, mafisadi, au kwenda kinyume na katiba, kufanya hivyo kuna hatari kubwa kwa mustakbali wa taifa.

Marjaa anasisitiza wasimamizi wa uchaguzi wafanye kazi kwa uaminifu, bila kushawishiwa na mali au siraha kinyume cha sheria au kuingiliwa na mataifa ya nje, waheshimu kazi yao na kulinda kura za wananchi hakika hiyo ni amana kwao. Na Mwenyezi Mungu ni mkuu wa kuwafikisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: