Atabatu Abbasiyya tukufu yawazawadia wahudumu wa kujitolea wa kitengo cha afya walioshiriki kwenye ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Idara ya afya katika Atabatu Abbasiyya tukufu imezawadia vijana waliojitolea kuhudumia mazuwaru wa Arubaini kutoka chama cha Imamu Hassan (a.s) katika mji wa Basra, walio ingizwa kwenye ratiba ya Ataba tukufu wakati wa ziara ya Arubaini, zawadi hizo zimetolewa katika nadwa iliyofanywa ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abbasi.

Kiongozi wa idara ya afya katika Atabatu Abbasiyya Dokta Osama Abdulhassan amesema: “Hakika sisi katika Atabatu Abbasiyya tunatoa shukrani za dhati kwa kazi tukufu iliyofanywa na vijana wetu waliojitolea kufanya kazi kwenye vituo vya afya ndani ya ukumbi mtukufu wa haram, chini ya ratiba ya afya ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wakati wa ziara ya Arubaini”.

Akaongeza kuwa: “Tumefanya kazi nyingi pomoja na vijana wa taasisi ya Imamu Hassan (a.s), ikiwa pia ni sehemu ya kujenga uwezo wa vijana hao, sambamba na kutoa huduma bora zaidi katika ziara zijazo”.

Kiongozi wa taasisi ya Imamu Hassan (a.s) Ustadh Haidari Aamiriy amesema kuwa: “Taasisi yetu kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu tumetoa huduma bora za afya kwa mazuwaru wa Arubaini”.

Akabainisha kuwa: “Taasisi ilianza kutoa huduma siku ya mwezi nane Safar, hadi mwisho wa ziara”. Akasifu, “Kazi kubwa iliyofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuwapa nafasi hiyo”.

Naye Ustadh Muhammad Karkuushi mmoja wa wahudumu wa kujitolea amesema: “Taasisi ya Imamu Hassan (a.s) imefanya kazi kubwa kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya kupitia idara ya afya, wametoa huduma za afya kwa watu wengi ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abbasi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: