Baadhi ya mitandao ya mawasiliano ya kijamii imerusha picha za kiongozi mkuu wa kisheria na muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani, zikionyesha Sayyid Swafi akiwa pamoja na ugeni wa viongozi wa makabila kutoka mkoa wa Ambaar miongoni mwa makumi ya ugeni rasmi na usiokua rasmi unaotembelea Ataba tukufu.
Kikao hicho cha wageni hao kilifanywa mwaka 2013m, kwa lengo la kuimarisha kuishi kwa amani na umoja wa kitaifa.
Tumeshangazwa na mitandao hiyo kwa kuandika uongo kuhusu kikao hicho, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya uandishi na hakuna faida yeyote, fungua link hii kuangalia yaliyozungumzwa kwenye kikao hizo: http://www.non14.net/public/43195
Tunapenda kukumbusha kuwa upokeaji wa ugeni wowote katika Atabatu Abbasiyya tukufu sio kibali cha utakaso au kukubaliana na mwenendo wa wageni hao, na sio sawa kuulizwa uongozi wa Ataba tukufu kuhusu mazungumzo yake na mgeni huyu au yule.