Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kinaendesha opresheni kubwa ya usafi

Maoni katika picha
Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, tangu asubuhi na mapema ya leo siku ya Jumatano, kimeanza kazi ya kusafisha eneo lote la katikati ya haram mbili na barabara zinazo elekea kwenye haram hizo na maeneo jirani, sambamba na kuondoa vifaa vyote vilivyowekwa kwa muda ili kuratibu matembezi ya mazuwaru na mawakibu zilizo shiriki kwenye ziara ya Arubaini.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafi Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tunafanya kazi hii baada ya kumaliza ziara ya Arubaini, hii ni hatua ya pili ambayo ni muendelezo wa hatua ya kwanza, tunafanya kila tuwezalo kurudisha mazingira katika hali ya awali, aidha hatua hii inakamilisha kazi ya usafi iliyofanywa kipindi chote za ziara”.

Akaongeza kuwa: “Kazi ya usafi imeanzia katika uwanja wa katikati ya haram mbili, kisha ikaendelea kwenye barabara zinazo elekea kwenye haram hizo na maeneo jirani, kama sehemu ya kusaidia harakati za watumishi wa Atabatu Abbasiyya na ofisi ya mkoa, tutaendelea kufanya usafi hadi tuzifikie sehemu zote tunazotakiwa kusafisha”.

Akasisitiza kuwa: “Katika kila msimu wa ziara watumishi wa kitengo chetu hufanya kila wawezalo katika kuwahudumia mazuwaru, husimamia usafi muda wote na kuweka mazingira mazuri ya kufanya ziara kwa amani na utulivu”.

Akamaliza kwa kusema: “Kazi yao haiishii kwenye kufanya usafi peke yake, bali wanaondoa baadhi ya vifaa vilivyowekwa kwa muda kwa ajili ya kuratibu matembezi ya mazuwaru na harakati za mawakibu za kuomboleza zilizo shiriki kwenye ziara ya Arubaini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: