Maelfu ya mazuwaru wameingia katika makumbusho ya Alkafeel wakati wa ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Maelfu ya mazuwaru wa Atabatu Abbasiyya tukufu wakati wa ziara ya Arubaini, wameingia katika makumbusho ya Alkafeel iliyopo ndani ya haram tukufu ya Abbasi, na kuangalia malikale za thamani zilizopo katika makumbusho hiyo.

Pamoja na kumiminika mazuwaru katika makumbusho hiyo kutoka mikoa tofauti ya Iraq, wameingia pia mazuwaru wa kiarabu na kiajemi, wamepongeza malikale walizoziona na namna zinavyo tunzwa na kuonyeshwa, sambamba na kuvutiwa zaidi na mambo yanayo husu haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama vile milango ya zamani, mabaki ya jingo yaliyotokana na shambulizi lililofanywa katika jingo hilo na utawala wa kidikteta uliopita.

Kumbuka kuwa makumbusho ya Alkafeel ni ya kwanza kufunguliwa katika Ataba tukufu za Iraq, ilifunguliwa mwaka (2009) wakati wa kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Zainabu (a.s), makumbusho hiyo inaidadi kubwa ya malikale, historia ya baadhi ya malikale hizo inarejea katika mamia ya miaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: