Upasuaji wa macho kwa mtoto mwenye umri wa miaka (3)

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel katika mji wa Karbala, kikosi cha madaktari wake kimefanikiwa kufanya upasuaji wa macho.

Jopo la madaktari limesema kuwa: “Kufaulu kwa upasuaji huu kunatokana na kuwepo vifaa vya kisasa katika hospitali ya Alkafeel, vinavyo lingana na vifaa vilivyoko kwenye hospitali kubwa za kimataifa”, akaongeza kuwa: “Tumefanikisha upasuaji bila kutokea tatizo lolote”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma bora kupitia vifaa tiba vya kisasa daima, chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo hilo limeiwezesha hospitali kutoa ushindani mkubwa kwenye hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel kila baada ya muda hualika madaktari bingwa wa fani tofauti, sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: