Mwezi ishirini na tatu Safar ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha mlezi wa Mtume wa mwisho na mzazi wa mbora wa mawasii

Maoni katika picha
Siku kama ya leo mwezi ishirini na tatu Safar ni kumbukumbu ya kifo cha bibi Fatuma binti Asadi bun Hashim bun Abdulmanafi, mama wa kiongozi wa waumini Ali (a.s) na mke wa Abu Twalibu (a.s), aliye kufa mwaka wa nne hijiriyya katika mji wa Madina.

Hunu ni mama mtukufu Mtume (s.a.w.w) anasema: (mama yangu baada ya mama), katika kuonyesha hadhi yake, kifo chake kilihuzunisha sana moyo wa Mtume (s.a.w.w), naye ni mtakatifu mama wa maimamu watukufu, bibi mwenye karama ya kupasuka ukuta alipoenda kujingua walii wa Mwenyezi Mungu, bibi mwenye Subira, mpiganaji, mdhulumiwa, mke wa muumini wa maquraishi mzee Abu Twalibu (a.s), dunia inahaki ya kuhuzunika na kuomboleza katika siku ya kifo chake.

Bibi mtukufu Fatuma binti Asadi bun Hashim bu Abdulmanafi ni mke wa Abu Twalibu (a.s) na mama wa kiongozi wa waumini (a.s), ni Hashimiyya wa kwanza kuolewa na Hashimiyya, alikua miongoni mwa watu wa kwanza kumuamini Mtume (s.a.w.w), kabla ya hapo alikua anafuata mila ya Ibrahim (a.s). alihama pamoja na Mtume (s.a.w.w), alikua mwanamke wa kwanza kula kiapo cha utii kwa Mtume (s.a.w.w) katika mji wa Maka baada ya bibi Khadija (a.s), naye ndiye mlezi wa Mtume (s.a.w.w).

Alikua sawa na mama mzazi wa Mtume (s.a.w.w), alilelewa na mama huyo, alikua anamheshimu sana na kumwita (mama yangu), alikua anamtembelea na kukaa katika nyumba yake.

Riwaya zinaonyesha kuwa Mtume (s.a.w.w) alimvisha sanda kwa kanzu yake, kisha akasema: (Hakika Jibrilu -a.s- aliniambia kutoka kwa Mola wangu mtukufu kuwa ataingia peponi, Mwenyezi Mungu aliamuru Malaika elfu sabini wamswalie, kisha akamswalia swala ya maiti, akashindikiza jeneza lake hadi kwenye makaburi ya Baqii na akamuweka kwenye mwanandani, halafu akamfunika kwa udongo kisha akatoka ndani ya kaburi.

Miongoni mwa umaalum wa bibi Fatuma binti Asadi (a.s) imepokewa ziara yake maalum, tofauti na wakina mama wengine watukufu ispokua Swidiqatu-Zzaharaa (a.s) na bibi Narjisi (a.s), miongoni mwa mambo yanayo onyesha hadhi yake ni maneno matukufu yaliyopo kwenye ziara yake.

Alikufa mwezi ishirini na tatu Safar mwaka wa (4h) katika mji wa Madina, kaburi lake lipo Baqii karibu na makaburi ya wajukuu zake Maimamu wa Baqii (a.s). amani iwe juu yake siku aliyozaliwa na siku aliyokufa na siku atakayo fufuliwa na kuwa hai kwa idhini ya Mola wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: