Watumishi wa idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanaendelea na kazi ya kusafisha baada ya kumaliza ziara ya Arubaini.
Kiongozi wa idara hiyo bwana Muhammad Ahmadi Jawadi amesema: “Baada ya kumaliza ziara ya Arubaini watumishi wetu wameanza kusafisha maeneo yote yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu na barabara zinazo elekea katika Ataba”.
Akaongeza kuwa: “Watumishi wetu wamezowea kufanya kazi hii kila mwaka baada ya kumaliza msimu wa ziara wakitumia vifaa vyote”. Akasema: “Kazi haijaishia kwenye mji mkongwe na maeneo yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya peke yake, bali tumesafisha sehemu zoto za malango ya mji na barabara zake”.
Akaendelea kusema: “Tunafanya kazi (saa 24) kwa kutumia vifaa tofauti hadi tutakapo maliza kusafisha sehemu zote tunazotakiwa kufikiwa”.
Kumbuka kuwa idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya kazi kubwa katika siku zote za ziara ya Arubaini.