Mateka wa nyumba ya Mtume warudi Madina

Maoni katika picha
Imeandikwa katika kitabu cha Asraar-Shahaadah: Imepokewa kuwa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) waliomboleza mbele ya kaburi la Hussein (a.s) kwa muda wa siku tatu, ilipofika siku ya nne wakaondoka kwenda Madina.

Walikaa siku tatu katika mji wa Karbala wakilia na kuomboleza hadi sauti zao zikakauka, Imamu Zainul-Aabidina (a.s) akaogopa kutokana na hali ya shangazi yake Zainabu na wanawake wengine, akaamuru waondoke kuelekea Madina, wakaondoka Karbala huku wanalia na kuomboleza.

Wengine wanasema: Kisha Ali bun Hussein (a.s), akaamuru msafara uondoke, Sukaina akaita kwa nguvu wakati wa kuaga kaburi la baba yake na akalia sana huku anasema:

Tambua ewe Karbala tunakuachia miili iliyozikwa bila sanda wala kuoshwa.

Tambua ewe Karbala tunakuachia roho ya Ahmadi na wasii pamoja na muaminifu.

Baadhi yao walimuambia Ali bun Hussein (a.s): Acha wanawake wawalilie ndugu zao. Akasema: Enyi watu hakika nyie hamuoni ninachoona, mimi naogopa shangazi yangu Zainabu asife, hakika anaenda kwenye kaburi baada ya kaburi akiwa anabuluza uso wake chini kwa ajili ya kumlilia ndugu yake Hussein..

Bibi Zainabu (a.s) alipoambiwa simama tuondoke.. alisema, twende wapi? Akaambiwa: Madina. Akasema: Nani aliyebaki Madina?

Msafara wa mateka wa Ahlulbait (a.s) ukaondoka kuelekea Madina, wakaondoka kwa unyonge huku macho yao yakiwa yamejaa machozi, wanawalilia ndugu zao waliouawa na kukumbuka udhalili waliopata, wakazi wa Madina walikusanyika kwenye msiba wa Ummu Salamah mke wa Mtume (s.a.w.w) aliyefariki mwezi mmoja baada ya kifo cha Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: