Zaidi ya sahani milioni za chakula zimetolewa na mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa idadi ya sahani za chakula kilichotolewa kwa mazuwaru wa Arubaini zilifika (1,217,457) milioni moja laki mbili elfu kumi na saba mia nne hamsini na saba, kuanzia siku za kwanza za ziara hadi kuondoka kwa zaairu wa mwisho, ugawaji wa chakula umefanywa kwa kufuata kanuni zote za afya za kujikinga na maambukizi.

Hayo yameripotiwa kwenye mtandao wa Alkafeel na rais wa kitengo Mhandisi Aadil Hamami, akaongeza kuwa: “Maandalizi ya ziara ya Arubaini mwaka huu yalianza mapema, tuliweka utaratibu maalum tukaandaa chakula na ratiba ya ugawaji pamoja na kubaini sehemu za kugawia, tumetumia vitendea kazi vyote vya mgahawa katika kufanikisha kazi hiyo”.

Akabainisha kuwa: “Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya huwa wa kwanza kutoa chakula kwa mazuwaru tangu siku za kwanza za mwezi wa Safar, wakati ambapo mawakibu za kutoa huduma huwa zipo kwenye kujiandaa na ziara, hivyo mgahawa huanza kugawa chakula mapema na huendelea hadi zaairu wa mwisho, tuliendelea kugawa hadi mwezi ishirini na moja Safar”.

Akafafanua kuwa: “Tunagawa chakula milo mitatu kila siku, ambayo ni (asubuhi, mchana na jioni), tunagawa chakula cha aina tofauti kulingana na mahitaji ya zaairu, pamoja na matunda, maji, juisi na vinginevyo, ambavyo hutolewa siku nzima, pamoja na kuchukua tahadhari za afya kwa kujikinga na maambukizi ili kulinda usalama wa wahudumu na mazuwaru watukufu”.

Akaendelea kusema: “Tumegawa chakula kupitia sehemu kuu nne zilizokua na msongamano mkubwa wa mazuwaru, kwa lengo la kufikia idadi kubwa zaidi bila kusababisha msongamano wakati wa kugawa chakula, tunagawa kupitia mstari wa wanaume na wanawake, ugawaji wa chakula ulikua unaongezeka kila siku hadi kufikia siku za kilele cha ziara”.

Akasema: “Hatukugawa chakula kwa mazuwaru peke yake, bali tuliwapa pia askari na wahudumu wa kujitolea waliokuja kushiriki kwenye ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akamaliza kwa kusema: “Mgahawa umeshiriki kupeleka wahudumu kwenye migahawa ya Ataba mbili tukufu na maukibu ya Ummul-Banina (a.s) wanaosaidia kuandaa na kugawa chakula kwa mazuwaru”.

Kumbuka kuwa mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) unajulikana na kila zaairu kutokana na huduma unazotoa, watumishi wa mgahawa huo hufanya kazi kubwa katika kila tukio linalo husu Ahlulbait (a.s), hususan ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu ikiwemo ziara ya Arubaini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: