Idara ya Qur’ani tawi la wanawake imehitimisha ratiba ya ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Idara ya Qur’ani tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha ratiba yake katika ziara ya Arubaini, iliyokua na vipengele tofauti katika kuhudumia mazuwaru watukufu.

Kiongozi wa idara amesema kuwa: “Idara ilikua na sehemu mbili kuu katika kuhudumia mazuwaru, zano ni sehemu ya moja kwa moja, idara iliunda kikosi kilichozunguka kwenye maeneo wanakopatikana mazuwaru katika Atabatu Abbasiyya na kuwafundisha usomaji sahihi wa surat Fat-ha, kipengele hicho kilipata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru, na walifurahishwa na njia iliyotumiwa na idara ya Qur’ani”.

Akaongeza kuwa: “Sehemu nyingine ilihusu uandaaji wa mihadhara kwa maandishi, iliyohusu ibada, maadili, aqida kwa kutumia aya za Qur’ani tukufu”.

Akabainisha kuwa: “Uwepo wao ulikua na athari kubwa katika nafsi wakati wa kusoma surat Fat-ha na kuelekeza thawabu zake kwa Ummul-Banina (a.s), na kuandika jina la zaairu kwa ajili ya kuliweka kwenye dirisha la kaburi kwa ajili ya kukidhiwa haja”.

Akasema: “Idara imetoa huduma tofauti za Qur’ani na kuelekeza thawabu kwa bwana wa mashahidi (a.s) na wafuasi wake, kwa njia ya mtandao na karatasi kwa kugawa majuzuu, pamoja na machapisho mengine yaliyo andaliwa na idara ya Qur’ani, miongoni mwa faida walizopata mazuwaru ni kuchukua sehemu ya nakala za machapisho hayo zilizokua na maudhui muhimu kwao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: