Kiongozi wa idara hiyo Mhandisi Farasi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Pamoja na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, tumeweka mkakati wa kuhakikisha tunapata kiwango cha barafu kinachohitajika, sambamba na hilo watumishi wetu walianza kazi mapema ya kutengeneza na kuhifadhi barafu, kwa ajili ya kuhakikisha hautokei upungufu wowote wa barafu kipindi cha ziara, pamoja na kuongezeka mahitaji ya barafu kutokana na kuongezeka kiwango cha joto”.
Akaongeza kuwa: “Barafu zilizozalishwa zilisambazwa kwenye maeneo yafuatayo:
- - Majengo yote ya kuhudumia mazuwaru yaliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Mawakibu zote za kutoa huduma zilizopo kwenye barabara zinazotumiwa na mazuwaru.
- - Idara ya maji chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, kwa lengo la kupoza maji ya kunywa wanayo pewa mazuwaru wa malalo takatifu, pamoja na maji wanayogawa kwa mawakibu na kwenye vituo vilivyo karibu yao na wakazi wa mji mkongwe.
- - Vikosi vya askari vilivyopewa jukumu la kulinda mazuwaru wa ziara ya Arubaini”.
Kumbuka kuwa kiwanda cha barafu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ni sehemu ya mkakati wa utumishi, unaolenga kuhudumia mazuwaru na wageni wanaokuja katika Ataba tukufu za Karbala na wakazi wa mji huo kwa ujumla, kiwanda kipo katika kituo cha (R.O) kwenye jengo la Saqaa/2 (magodauni ya Atabatu Abbasiyya tukufu), kinazalisha barafu kisasa na zenye ubora mkubwa.