Shindano linahusisha vipande vya video vilivyo rekodiwa mambo yanayo endana na utamaduni wa Husseiniyya yanayo onyesha matendo ya kibinaadamu na kiislamu katika matembezi ya Arubaini chini ya mada zifuatazo:
- Usafi na muonekano wa utamaduni wa Husseiniyya.
- Kazi za kujitolea na kusaidiana kijamii.
- Hijabu na utamaduni wa Zainabiyya.
- Picha ya malezi ya Husseiniyya katika mwenyendo wa watoto.
- Muonekano wa kulinda neema na kutofanya ubadhirifu.
Chini ya kanuni zifuatazo:
- Kipande cha video kisizidi dakika tatu.
- Unaweza kuandaa video na kuipeleka kwenye kamati inayohusika na video.
- Muonekano wa picha usiwe chini ya 1mb, hakikisha video inamuonekano mzuri.
- Isiwe na nembo yeyote au alama ya kibiashara.
- Picha zisiwekwe kitu chochote, kama maandishi, nembo na alama.
Masharti ya shindano:
- Mshiriki anahaki ya kutuma picha moja au mbili.
- Mshiriki haruhusiwi kutuma video zaidi ya moja.
- Video iwe haijawahi kuonekana sehemu nyingine, au kushiriki kwenye shindano lingine.
- Maktaba inahaki ya kutumia itakavyo.
- Mshiriki anahaki ya kunufaika na kazi yake katika upande wa usanifu, kwenye majarida na sehemu zingine.
- Kazi zote zitawasilishwa kwenye kamati ya majaji watakao chuja na kupata washindi watano upande wa sauti na watano upande wa video.
- Kazi hizo zitawekwa kwenye mtandao maalum wa maktaba.
- Majina ya washindi yatatangazwa mwezi (9 Ribiul-Awwal 1443h) sawa na tarehe (16 Oktoba 2021m).
- Washindi watano wa mwanzo katika kila kipengele watapewa zawadi.