Kamati inayoratibu vituo vya kijana wa Alkafeel kwa wanafunzi wa vyuo na shule za sekondari (upili), wametangaza majina ya waliofaulu kwenye shindano lililofanywa wakati wa ziara ya Arubaini na kushiriki zaidi ya mazuwaru (4000), majibu sahihi yalifika (318) yakapigiwa kura ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kupata washindi (20).
Kituo kilikua kinahusu maadili na utamaduni kwa mazuwaru watukufu, kwa lengo la kuongeza maarifa kwa kundi la vijana, jumla ya vitengo nane vya Atabatu Abbasiyya tukufu vilishiriki kwenye program hiyo, vilikua na matawi ishirini yaliyoweka kambi katika chuo kikuu cha Al-Ameed kwenye (maukibu ya Ummul-Banina a.s) iliyopo barabara ya Najafu – Karbala.
Kumbuka kuwa mazuwaru walipewa maswali moja kwa moja, yalikua yanahusu harakati ya Imamu Hussein (a.s).
Kwa ajili ya kuwasiliana na kamati iliyoratibu na kusimamia shindano, ili kupokea zawadi, tunawaomba waliofaulu wapige simu kwa namba (07718269319).