Kazi ya kusafisha na kutandika mazulia ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) jioni ya jana siku ya Jumapili, wameanza kazi ya kusafisha haram tukufu na kutandika mazulia baada ya kuisha msimu wa ziara ya Arubaini.

Kazi hiyo imefanywa na watumishi wa idara ya wasimamizi wa hara tukufu, pamoja na wahudumu kutoka kitengo cha utumishi na masayyid wanaotoa huduma, mbele ya mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Dhiyaau-Dini na baadhi ya marais wa vitengo.

Kiongozi wa idara ya haram bwana Nizaar Ghina Khaliil ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya kumaliza ziara ya Arubaini tumesafisha na kutandika mazulia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), tumezowea kufanya kazi hii katika siku kama hizi, kabla ya kuanza kazi hiyo tulisoma ziara ya mwenye malalo tukufu kwa pamoja, kama ishara ya kuomba ruhusa ya kufanya kazi hiyo.

Akaongeza kuwa: “Kazi tulizofanya zimehusisha kutandua mazulia na kusafisha kuanzia sehemu lilipo kaburi takatifu na maeneo yanayo zunguka sehemu hiyo hadi kwenye korodo nne na kuta zake, tumetumia maji ya dawa yenye uwezo wa kuondoa uchafu na kuua bakteria wasababishao maambukizi, tukamalizia kwa kupuliza marashi na kutandika mazulia kwa kufuata vipimo tulivyokua tumesha chukua kulingana na kila zulia na sehemu yake”.

Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Zainul-Aabidina Adnani akaongeza kuwa: “Hakika haram tukufu imeshuhudia kazi ya kutandua mazulia yaliyotandikwa wakati wa ziara, na kwenda kuyaosha kwenye kituo kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kisha tukaanza kazi ya kusafisha iliyofanywa kwa kuzingatia kila sehemu ya haram tukufu, baada ya kumaliza kufanya usafi tumetandika mazulia mapya na kurudisha mazingira ya haram tukufu kama yalivyokua awali sambamba na kuweka vitabu vya ziara na dua”.

Kumbuka kuwa ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi -a.s- husafishwa kila wakati ndani ya mwaka mzima, lakini kila baada ya kumaliza msimu wa ziara kubwa ikiwemo ziara ya Arubaini, hufanywa usafi wa kina unao husisha watumishi kutoka vitengo tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: