Mavuno zaidi ya tani saba za tende katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu

Maoni katika picha
Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kupitia idara ya miti na mapambo, kimevuna tende zilizopo katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wamepata kiwango cha kilo (7500), wamezisafisha na kuziweka kwenye vifungashio kisha zitagawiwa kwa mazuwaru bure.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kitengo chetu kupitia idara ya kilimo inaipa kipaombele zaidi bustani iliyopo katikati ya haram mbili tukufu, ambapo miti ya mitende kwenye eneo hilo ni alama kuu na urembo, mwisho wa kila msimu huwa tunavuna tende na kuzikusanya sehemu moja, kisha husafishwa na kuondoa zisizofaa halafu huwekwa kwenye vifungashio maalum kwa ajili ya kuzigawa bure kwa mazuwaru kama sehemu ya kutabaruku na sehemu hiyo takatifu”.

Kiongozi wa idara ya miti na mapambo Mhandisi Haatim Abdulkarim Habibu amesema: “Kazi ya idara yetu imegawika sehemu tofauti, zote zinalenga kudumisha muonekano wa kijani kibichi katika eneo hilo, miti ya mitende inanafasi kubwa katika kuhakikisha jambo hilo, ni aina nzuri na inapendwa, kuna ratiba maalum ya kuichambulia na kuisamadia pamoja na kuipulizia dawa, sambamba na kuisafisha.

Akafafanua kuwa: “Baada ya tende kuiva huvunwa na kukusanywa sehemu moja, kisha hufungwa kwenye vifungashio vidogo ambavyo huandikwa jina la kitengo, baada ya hapo hugawiwa bure kwa mazuwaru kama zawadi za kutabaruku, mwaka huu tumezigawa katika mwezi wa Muharam, tuliwapa mazuwari, mawakibu Husseiniyya na wenye maambukizi ya virusi vya Korona”.

Kumbuka kuwa miti ya mitende iliyopandwa kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, ni moja na miti muhimu inayoweka muonekano wa kijani kibichi katika eneo hilo, sambamba na umuhimu wake, miti hiyo ipo (57) kama ishara ya umri wa Imamu Hussein (a.s) aliokua nao siku ya kifo chake katika vita ya Twafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: