Atabatu Abbasiyya tukufu imejiandaa kupokea siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya kumaliza msimu wa ziara ya Arubaini, imeanza kujiandaa kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya msiba mkubwa zaidi katika nyoyo za waumini na umma wa kiislamu, nayo ni kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), siku aliyokufa inasadifiana na mwezi (28) Safar.

Miongoni mwa maandalizi yanayo ingia katika ratiba ya uombolezaji, ni kuweka mapambo yanayoashiria huzuni na uombolezaji kwenye korido zote za malalo tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mazingira yaliyoanza kuonekana toka mwezi mosi Muharam, muonekano wa huzuni huendelea hadi katika siku hiyo.

Katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume mtukufu, Nabii wa rehema na muombezi wa umma Muhammad bun Abdallah (s.a.w.w), kila sehemu huongezwa mapambo yanayo ashiria huzuni, kwa ajili ya kuomboleza msiba unaoumiza zaidi umma wa kiislamu, alama kuu zinazo ashiria huzuni zimewekwa kwenye mlango wa Kibla wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwenye milango ya haram yake takatifu, kama sehemu ya kuonyesha kuanza kwa msimu wa huzuni za kifo cha Mtume, pamona na sehemu zingine ndani na nje ya haram tukufu.

Ratiba iliyoandaliwa kwa ajili ya maombolezo hayo inakipengele cha mihadhara ya kidini, na kupokea mawakibu za kuomboleza zinazokuja kumpa pole mjukuu wake Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na mambo mengine ya uombolezaji.

Kumbuka kuwa Mtume Muhammad bun Abdallah (s.a.w.w) alifariki tarehe (28) Safar mwaka wa 11 hijiriyya, akiwa na umri wa miaka 63, wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika siku hiyo huenda kuzuru kaburi la simba wa Mwenyezi Mungu mwenye kushinda Ali bun Abu Twalib (a.s) kumpa pole kwa kufiwa na kipenzi wake, kaka yake mtoto wa Ammi yake Mtume wa rehema Muhammad (s.a.w.w), nayo ni miongoni mwa ziara maalum, asilimia kubwa ya mazuwaru wakimaliza ziara hiyo huenda Karbala kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: