Katika siku kama ya leo dunia ilijaa giza kwa kifo cha kiumbe ambaye kwa sababu yake viumbe waliumbwa

Maoni katika picha
Jumatano mwezi kumi na nane Safar ni siku aliyofariki kiumbe bora zaidi, na mbora wa mitume Muhammad (s.a.w.w), mwaka wa 11 hijiriyya akiwa na umri wa miaka 63.

Dunia ilijaa giza kwa kufa mtu ambaye kila kitu kiliumbwa kwa ajili yake, Jibrilu akaondoka na ukawa mwisho wa kushuka wahyi katika ardhi, ardhi takatifu ikabaki pweke, Utume ukafungwa, hakuna tena mtume baada ya leo, hakika hii ni siku ngumu sana.

Ali (a.s) alikua mtu wa karibu sana kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, alikua pembeni yake wakati wa kifo chake, anasema: “…Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alifariki kichwa chake kikiwa kifuani kwangu, nafsi yake ilitoka akiwa mikononi mwangu, nyumba ikajaa vilio, huku Malaika wanashuka na kupanda, masikio yangu hayakuacha kusikia Malaika wanavyo mtakia rehema hadi tulipomuweka kaburini”, hapo kiongozi wa waumini Ali (a.s), alipenda kuonyesha ushiriki wa Malaika katika maziko ya Mtume (s.a.w.w), nyumba ilijaa Malaika waliokua wanalia na kuomboleza kifo cha Mtume mtukufu.

Kiongozi wa waumini akaeleza mazingira ya kumuandaa na kumzika, akasema: “Nilikua mtu wa mwisho katika maandalizi ya maziko yake” baada ya kuchimbwa mwanandani, kiongozi wa waumini akaingia kupokea muili wake (s.a.w.w), akampokea na kumuweka mikononi mwake, akafunua uso wa Mtme (s.a.w.w), akaweka shavu lake juu ya ardhi akiwa ameelekea Kibla, kisha akafunikwa udongo.

Baada ya kazi hiyo kiongozi wa waumini Ali (a.s) alilia na kutokwa machozi kwa kuondokewa na ndugu yake Muhammad bun Abdullahi Mtume muaminifu (s.a.w.w), alipata uchungu mkubwa katika msiba huo, alisimama pembeni ya kaburi la ndugu yake akiwa anatikisa kichwa, huku machozi yanashuka kwenye mashavu yake na anasema: “Kwa haki ya baba wewe na mama ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kifo chako kimeondoa mambo ambayo hayajawahi kuondoka kwa kifo cha Mtume yeyote, watu wote kwako walikua sawa, lau kama usingeamrisha subira na ukakataza pupa tungefanya mambo yasiyofaa”.

Riwaya zinaonyesha kuwa kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s) aliomboleza kifo cha Mtume (s.a.w.w) kwa kusema:

Hivi baada ya kumvisha sanda Mtume na kumzika tutahuzunika kwa kifo cha mwingine.

Tulipewa Mtume wa Mwenyezi Mungu asiyekua na mbadala ulimwenguni.

Amerithiwa na mtoto wake Fatuma Zaharaa (a.s) kwa kauli yake:

Muambie aliyetoweka chini ya udongo kama unasikia sauti na wito wangu.

Nimefikwa na misiba lau ingeisibu michana ingekua usiku.

Nitafanya kukuhuzunikia ndio liwazo langu, na kukulilia ndio furaha yangu.

Inakua vipi kwa mtu aliyenusa udongo wa Ahmadi, hawezi kunusa tena kingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: