Kituo cha turathi za Karbala kinafanya kazi kubwa ya kuhakiki turathi

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya kazi kubwa ya kielimu katika sekta ya uhakiki, uandishi na utafiti.

Hivi karibuni kituo kinatarajia kutoa vitabu tofauti ilivyo hakiki, ikiwa ni pamoja na nakala ya ishirini na saba na ishirini na nane ya jarida la (Turathi za Karbala), lenye tafiti nyingi za turathi na fiqhi.

Miongoni mwa vitabu vitakavyo kamilka hivi karibuni ni kitabu cha (Uwa lichanualo katika maarifa ya majazi na uhakika), baada ya watumishi wa kituo kuhakiki na kuweka faharasi, nacho kimeandikwa na Allamah Mhakiki Faqihi Sayyid Muhammad Baaqir Mussawi Shaftiy, na kuhakikiwa na Sayyid Muhammad Ridhwa Shaftiy.

Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya kazi ya kukusanya na kupanga kila kitu kinacho husiana na turathi za mji mtukufu wa Karbala, kimechapisha vitabu vingi na nyaraka mbalimbali zilizo fanyiwa uhakiki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: