Kitengo cha malezi na elimu ya juu kinafanya nadwa kwa watumishi wa shule za awali za mayatima katika mji wa Najafu

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya nadwa kwa watumishi wa shule za awali Alkafeel za mayatima katika mji wa Najafu, chini ya harakati za kusaidia taasisi za malezi na elimu katika mji huo.

Nadwa inamada tofauti zinazolenga kujenga uwezo wa walimu na kuwafundisha mbinu za ufundishaji wa kisasa.

Mada ya kwanza imewasilishwa na Dokta Imadu Dhwalimi ilikua inasema (changamoto za kusoma), inalenga kuwajengea uwezo wa kubaini changamoto za kusoma walimu ya shule za awali, naye Ustadh Hassan Juma akawasilisha mada ya pili isemayo (namna ya kupambana na changamoto), kwa lengo la kuwajengea walimu uwezo wa kupambana na changamoto za watoto, hakika kila mtoto anachangamoto yake.

Mada ya tatu imetolewa na Ustadh Abdulhussein Yahya, ilikua inasema (Mazingira ya darasa), ilihusu kugawa darasa kwenye nguzo kuu nne, nguzo ya mama, nguzo ya familia, nguzo ya ufundi, nguzo ya elimu, jambo hilo linaweka mazingira mazuri ya malezi na ufundishaji watoto darasani.

Tambua kuwa kitengo cha malezi na elimu ya juu, kinazingatia uendeshaji wa semina, warsha na mashindano ya kielimu, kwa lengo la kujenga uwezo wa walimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: