Kuzawadia vikundi 17 vilivyosaidia kutekeleza ratiba ya kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili wakati wa ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya kimezawadia vikundi (17) vya Husseiniyya, vilivyo saidia utekelezaji wa ratiba yake ya kuhudumia mazuwaru wakati wa ziara ya Arubaini, jumla ya watu (2200) wameshiriki kutoa huduma chini yake, zawadi hiyo ni sehemu ya kutambua na kuthamini kazi kubwa waliyofanya bega kwa bega na watumishi wa kitengo.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Zawadi hizi ni sehemu ya kutambua na kuthamini kazi kubwa iliyofanywa na watu waliojitolea, walikua msaada mkubwa kwa watumishi wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, katika kutekeleza majukumu yao wakati wa ziara ya Arubaini”.

Akaongeza kuwa: “Wahudumu wa kujitolea wamefanya kazi kubwa katika sekta tofauti, ikiwemo sekta ya kuratibu matembezi ya mazuwaru na mawakibu, na kuhakikisha hakutokei msongamano, pia kunawaliofanya kazi ya usafi na kuandaa sehemu za kupumzika mazuwaru, pamoja na kuweka vitu wanavyo hitaji mazuwaru wakati wa ziara”.

Wahudumu wa kujitolea wameshukuru kupewa nafasi ya kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wakasema kuwa hilo ni jambo kubwa sana kwao, sambamba na kupewa heshima nyingine tukufu na uongozi wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili kwa kuwapa zawadi hii, tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe umri mrefu ili tuweze kushiriki katika ziara zingine zijazo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: