Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), ndani ya sardabu ya Mussa Alkadhim (a.s), na kuhudhuriwa na mazuwaru na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Ratiba hiyo imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na muhadhara uliotolewa na mmoja wa wahadhiri wa idara, ameongea kuhusu historia ya Mtume (s.a.w.w), akaeleza sifa za Mtume (s.a.w.w) na mazingira ya wakazi wa Maka na maadili ya watu wa kipindi cha Mtume (s.a.w.w), akasema kuwa tabia za Mtume na hekima yake ulikua msaada mkubwa katika ulinganiaji wake, akahitimisha kwa kusoma tenzi za msiba na mambo waliyokutana nayo watu wa nyumba ya Mtume (a.s) baada ya kifo chake.
Mwisho wa majlisi hiyo zikatumwa salamu za rambirambi kwa Imamu wa zama (a.f), na ikasomwa dua ya Faraj sambamba na kuuombea dua umma wa kiislamu na dunia kwa ujumla, Mwenyezi Mungu atujaalie afya na amani.