Dondoo ya kumbukumbu ya kulala kwa kiongozi wa waumini Ali katika tandiko la Mtume (s.a.w.w)

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa Jibrilu (a.s) alimuambia Mtume (s.a.w.w) kuwa Mwenyezi Mungu anamuamuru ahame kwenda Madina, akamwita (s.a.w.w) kiongozi wa waumini Ali (a.s) akamuambia hilo, akasema (s.a.w.w) kumuambia: (Mwenyezi Mungu Mtukufu ameniamuru nikuamrishe ulale kwenye tandiko langu, uwepo wako ufiche kutokuwepo kwangu, unaonaje?), tukio hilo lilitokea usiku wa kwanza wa mwezi wa Rabiul-Awwal mwaka wa (13) wa Utume mtukufu.

Kiongozi wa waumini Ali (a.s) akasema: (Utasalimika kwa kulala kwangu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?). akasema (s.a.w.w): (Ndio..).

Akatabasamu Imamu (a.s) na akacheka, kisha akasujudi. Usiku huo kiongozi wa waumini (a.s) akalala kwenye tandiko la Mtume (s.a.w.w) akiwa amejiandaa kuuawa.

Wakaja makuraishi kutekeleza njama yao, walipotaka kumkata panga wakiwa wanaamini kuwa ni Muhammad (s.a.w.w), wakamuamsha, wakakuta ni Imamu Ali (a.s) wakamuacha, na kwenda kumtafuta Mtume (s.a.w.w).

Kabla ya kuondoka Mtume (s.a.w.w) aliwasiliana na kiongozi wa waumini Ali (a.s), akamuamuru aende Maka na atangaze: (Yeyote aliyekua na amana kwa Muhammad aje nimrudishie amana yake). Kisha akasema (s.a.w.w): (Hakika hawatakufanyia jambo baya ewe Ali, hadi utakapokuja kwangu, rudisha amana mbele ya macho ya watu kwa uwazi).

Baada ya Mtume (s.a.w.w) kufika Madina, alimuandikia kiongozi wa waumini Ali (a.s) barua aliyomuamuru amfuate.

Fakhru Razi katika Tafsirul-Kabiir kwenye tafsiri ya aya isemayo (Miongoni mwa watu wapo wanao uza nafsi zao kutafuta radhi ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni mpole kwa waja), amesema: sababu ya kushuka aya hiyo ni Ali bun Abu Twalib (a.s), alilala kwenye tandiko la Mtume (s.a.w.w) usiku aliotoka kwenda kwenye pango.

Akasema: imepokewa kuwa, alipolala kwenye tandiko la Mtume (s.a.w.w), Jibrilu alisimama upande wa kichwa chake, na Mikaeli upande wa miguuni kwake, Jibrilu alikua anasema: Hongora (Bakh-Bakh..) nani mfano wako ewe mtoto wa Abu Twalib, Mwenyezi Mungu na Malaika wanakupongeza, ndipo ikashuka aya tuliyotangulia kuisoma.

Hakika kulala kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s) kwenye tandiko la Mtume Muhammad (s.a.w.w) halikua jambo jepesi linaloweza kufanywa na mtu yeyote wa kawaida, lilikua jambo linalohitaji ushujaa mkubwa, hususan anapotambua kuwa lazima atauawa, kwani Makuraishi walikua wameamua kuangamiza Dini na kumuua Mtume Mtukufu katika usiku huo, lakini Mtume alifanikiwa kuondoka usiku bila kuonekana na mtu yeyote, huku akisoma maneno ya Mwenyezi Mungu yasemayo: (Tukaweka kizuwizi mbele yao na kizuwizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hiyo hawaoni), na kwa msaada wa kiongozi wa waumini aliyelala kwenye tandiko lake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: