Baada ya swala Maghribaini siku ya Alkhamisi (29 Safar 1443h) sawa na tarehe (7 Oktoba 2021m), imebadilishwa bendera ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imetolewa nyeusi na kuwekwa nyekundu, kama ishara ya kumaliza msimu wa huzuni wa mwezi wa Muharam na Safar, na tangazo la kuingia mwezi wa Rabiul-Awwal ambao umeonekana leo jioni.
Kubadilisha bendera hiyo ni utamaduni uliozoweleka katika kupokea mwezi wa Rabiul-Awwal, kundi la watumishi wa Atabatu Abbasiyya limefanya kazi ya kuondoa mapambo meusi yaliyokua yamewekwa kwenye minara na mabango meusi yaliyokua yamewekwa kila sehemu ya haram tukufu, kisha wakaenda katika uzio wa nje na kutoa vitambaa na mabango yote meusi.
Kumbuka kuwa bendera nyeusi itaendelea kupepea juu ya kubba takatifu kwa muda wa miezi kumi, inamaanisha kuwa mwenye kaburi hili aliuawa na bado hajalipiwa kisasi, na bendera nyeusi humaanisha kuwa siku hizi ndio alizouawa mwenye kaburi hili, ndio maana huwekwa juu ya kubba la bwana wa mashahidi Imamu Hussein na kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mwezi wa Muharam na Safar.