Idara ya Qur’ani imetangaza majina ya washindi wa shindano la (Huwezi kufuta utajo wetu) na (Fajrul-Hussein -a.s-)

Maoni katika picha
Idara ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza majina ya washindi wa shindano la (Huwezi kufuta utajo wetu) na (Fajrul-Hussein a.s).

Kwenye shindano la (Huwezi kufuta utajo wetu) ambalo ni shindano la kuhifadhi hutuba ya bibi Zainabu (a.s) aliyotoa katika kikao cha Yazidi (Allah amlaani) wameshiriki watu (80), washindi watatu wa mwanzo ni:

Mshindi wa kwanza: Wasan Nuuri Hussein kutoka Karbala.

Mshindi wa pili: Saja Ali Abdu kutoka Bagdad na Janaan Ibrahim Muhammad kutoka Karbala.

Mshindi wa tatu: Zainabu Atwiyya Abdul-Azizi kutoka Dhiqaar na Aayah Laiibi Madaah kutoka Bagdad pamoja na Jannaat Dhiyaau mwanafunzi wa darasa la tatu.

Amma shindano la (Fajrul-Hussein a.s) la kuhifadhi surat Fajri, washindi walikua wafuatao:

Mshindi wa kwanza: Mayamini Falaah Mustwafa kutoka Bagdad.

Mshindi wa pili: Sira Ra’adu Jaasim kutoka Najafu.

Mshindi wa tatu: Zainabu Muhsin Abdulkariim na Ruqayyah Muntadhwar Abdulhurru kutoka Najafu.

Idara inawaomba washindi wawasiliane nayo kwa ajili ya kuchukua zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: