Ugeni kutoka Boznia umetembelea makumbusho ya Alkafeel na kupongeza malikale zilizopo na mpangilio wa makumbusho hiyo

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Boznia unaojumuisha viongozi wa kisekula na wasomi, umetembelea makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuangalia malikale zilizopo kwenye makumbusho hiyo, ambazo historia ya malikale hizo inarejea katika miongo na vipindi tofauti.

Ugeni umesikiliza maelezo kutoka wasimamizi wa makumbusho, kuhusu malikale na namna ya utunzwaji wake, na maelezo ya kila aina na historia yake.

Wamefurahishwa na kuvutiwa na malikale walizoona katika makumbusho ya Alkafeel, sambamba na kupongeza kuzi kubwa inayofanywa na wahudumu wa makumbusho hiyo, katika sekta ya maonyesho na utunzaji wa malikale.

Mwisho wa matembezi yao rais wa ugeni huo Ustadh Kadhim Hajiliji -mkufunzi wa chuo kikuu cha falsafa kitengo cha masomo ya kiislamu nchini Baznia- ameshukuru sana kupewa nafasi ya kutembelea makumbusho ya Alkafeel, akafafanua kuwa: “Sina maneno nayoweza kutumia kuonyesha mapokezi mazuri tuliyopewa na huduma bora tulizo fanyiwa, namshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kutuwezesha kufika kwa watu wanaolinda misingi ya ubinaadamu”.

Kumbuka kuwa makumbusho ya Alkafeel hupokea wageni kila wakati kutoka taasisi za kielimu na viongozi tofauti wa ndani na nje ya Iraq, kutokana na malikale zilizopo kuwa na historia kubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: