Mpiga picha kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu amepata nafasi ya kwanza kwenye shindano la kimataifa la kupiga picha

Maoni katika picha
Mpiga picha wa kituo cha Alkafeel chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu bwana Azharu Hamidi Asadi, amekua mshindi wa kwanza kwenye shindano la Imamu Hussein (a.s) la kupiga picha za mnato awamu ya nane, linalofanywa katika nchi ya Baharaini chini ya kauli mbiu isemayo: (Ashura ni rehema kubwa) wameshiriki wapigapicha (110) kutoka nchi tofauti, jumla ya picha (385) zimeshiriki.

Asadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Wapiga picha wa kituo cha Alkafeel wana ujuzi na uzowefu mkubwa unaowawezesha kushiriki kwenye shindano lolote la kitaifa na kimataifa, na hupata nafasi za juu kwenye kila shindano, likiwemo shindano hili ambalo nimepata nafasi ya kwanza na kuweza kutoa ushindani kwa wapiga picha wengine wa kimataifa”.

Akaongeza kuwa: “Shindano linalenga kuonyesha matukio ya Ashura ya mwaka huu wa (1443h), katika mazingira magumu ambayo dunia inapitia kwa mwaka wa pili mfululizo, kutokana na kuwepo kwa janga la virusi vya Korona na kuheshimu umbali kati ya mtu na mtu katika mikusanyiko, kamera zimetakiwa kutuonyesha picha halisi za matukio tofauti, sambamba na ujumbe unaotolewa na picha hizo na malengo ya ujumbe huo”.

Akaongeza kuwa: “Picha niliyotumia niliipa jina la (Mapenzi ya Hussein a.s) ni picha inayomuonyesha mtoto ambaye wazazi wake wanashiriki kwenye maukibu ya kuomboleza ya Ashura, na inaonyesha uzingatiaji wa kazuni za afya na usalama kwa ujumla, ndipo kamati ya majaji ikaitunuku picha hiyo kwa kuipa ushindi wa kwanza”.

Kumbuka kuwa ushiriki wa shindano hili na kupata ushindi ni moja ya mfululizo wa zawadi nyingi wanazopata wapiga picha wa Atabatu Abbasiyya tukufu, saya yawe mashindano ya kitaifa au kimataifa, kutokana na ujuzi na uzowefu walionao unawapa nafasi ya kushinda, pamoja na msaada endelevu wanaopewa na viongozi wa kitengo hicho, bila kusahau uongozi wa juu wa Atabatu Abbasiyya, ambao unawapa kila aina ya kifaakazi wanacho hitaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: