Shuhudia.. dirisha la maqaam ya mkono baada ya kukamilika kuunganishwa kila kitu

Maoni katika picha
Kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango yake tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, kimesema kuwa mafundi wake wamemaliza kufunga dirisha la maqam ya mkono wa kushoto wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya uwanja wa kiwanda, huu ndio ufungaji wa mwisho kabla ya kwenda kuliweka sehemu yake rasmi nje ya uzio wa Atabatu Abbasiyya tukufu, mkabala na mlango wa kiongozi wa waumini (a.s).

Rais wa kitengo hicho na msimamizi wa kazi hiyo Sayyid Naadhim Ghurabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hatua ya ufungaji wa pili imekamilika baada ya kumaliza kuweka madini ya mina, dhahabu, mapambo na nakshi kama ilivyo pangwa, sambamba na kuzingatia ushauri wa kifundi, hii ndio kazi tuliyofanywa kwa sasa, tunamshukuru Allah kazi yote ya kuunganisha dirisha imekamilika bila tatizo lolote”.

Akabainisha kuwa: “Dirisha linapembe nane, nalo ni dirisha la kwanza kutengenezwa katika umbo hilo, linamzunguko wa (mita 3) na urefu wa (mita 2.85), umbo lake limetengenezwa kwa silva yenye ujazo wa (mlm 2), limesanifiwa na kutengenezwa kwa uhodari mkubwa, miongoni mwa sifa zake ni:

  • - Linamadirisha madogo madogo nane, yenye urefu wa (sm 190) na upana wa (mt 1), yanaviduara (176) na matundu (42) yaliyowekwa (21) kila upande, pamoja na mapambo ya pembe tatu yaliyo wekwa nakshi za mimea zinazo fanana na zile zilizopo kwenye dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Nguzo kuu zipo (8) kwenye mzunguko wa dirisha, zimenakshiwa na kuwekwa mapambo ya mimea, yapo pembeni ya nguzo za dirisha yamewekwa kwa muundo wa nguzo ndogondogu (16), kila nguzo moja imewekewa kitako cha pambo na taji.
  • - Ufito wa maandishi (ya Qur’ani) yenye urefu wa (sm 20) umezunguka dirisha pande zote, umeandikwa aya za surat Mutwafifiina, kuanzia (Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema…) hadi (… wakae juu ya viti vya enzi wanaangalia), umeandikwa kwa dhahabu iliyotiwa mina ya bluu, na kuna ufito kwa juu wa mapambo wenye upana wa (sm 6).
  • - Ufito wa maandishi ya (shairi) unaurefu wa (sm 20) miongoni mwa tungo za Ali Safaar, maandishi hayo yamezunguka dirisha pia, yameandikwa kwa maji ya dhahabu iliyotiwa mina ya kijani kwa upande wa juu ya dirisha.
  • - Ufito wa mapambo (urembo) uliozunguka pembe nane za dirisha, unaurefu wa (sm 28), kila sehemu inauwa la duara, kuna jumla ya mauwa (16), kila sehemu inatenganishwa na sehemu nyingine kwa urembo wa fedha uliowekwa kwenye nguzo zote nane za dirisha, urembo huo umewekwa katikati ya ufito wa maandishi ya Qur’ani na shairi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: