Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya, imefanya kikao cha pili kujadili uboreshaji wa harakati za Qur’ani katika wilaya hiyo na kwenye vitongoji vyake: (Qur’ani tukufu ni msingi wa Imani na ngao ya jamii).
Kikao kimejadili nukta nyingi muhimu kuhusu uboreshaji wa harakati za Qur’ani na namna ya kutatua changamoto, sambamba na kujadili mambo muhimu yanayofaa kufanywa siku za mbele katika sekta ya tafsiri na maarifa ya Qur’ani.
Tambua kuwa mkutano huu unafanywa kwa mara ya pili.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu kupitia matawi yake tofauti, inalenga kufundisha Qur’ani na kusaidia kuandaa jamii yenye uwezo wa kufanya tafiti katika sekta zote za Qur’ani tukufu.