Mkuu wa wahariri wa gazeti la (Minashi) mwandishi wa Habari kutoka Japani bwana Shinisako Manu ametembelea makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Wakati wa matembezi yake kwenye makumbusho hiyo amesikiliza ufafanuzi kutoka kwa wahudumu wa makumbusho, wameelezea malikale adimu zilizopo kwenye makumbusho hiyo na namna ya ukarabati na utunzwaji wake.
Muandishi huyo kutoka Japani amefurahishwa na malikale hizo, na akawatakia wahudumu mafanikio zaidi, akaonyesha furaha kubwa aliyonayo kwa kufanikiwa kutembelea Karbala, akaomba taifa la Iraq lipate amani na utulivu.
Kumbuka kuwa makumbusho ya Alkafeel hutembelewa na taasisi za aina tofauti pamoja na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Iraq, kutokana na malikale adimu na zenye historia kubwa ilizonazo.