Kuunganisha mfupa wa taya la chini la mgonjwa mwenye umri wa miaka 18

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limefanikiwa kuunganisha mfupa wa taya la chini la mgonjwa mwenye umri wa miaka 18.

Daktari bingwa wa upasuaji wa uso katika hospitali hiyo Dokta Ridhwani Twaaiy amesema: “Mgonjwa alikua na maumivu makali ya uso, vipimo vikaonyesha amevunjika mifupa miwili kwenye taya ya chini”, akaongeza kuwa: “Tumemfanyia matibabu ya kuunganisha mfupa kwa kutumia kifaa maalum ambacho hutumiwa kwa wagonjwa wa aina hiyo, bila kupasua mdomo, nayo ni njia ya kisasa ambayo hutoboa sehemu ndogo sana ndani ya mdomo”.

Akasisitiza kuwa: “Kuwepo kwa vifaa vya kisasa katika hospitali ya rufaa Alkafeel kumesaidia kwa kiwango kikubwa kufanyika kwa matibabu ya aina hii”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hutoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa vya kisasa, kutokana na uwepo wa vifaa vivyo na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa waliobobea katika fani tofauti kila baada ya muda, sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali mbalimbali za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: