Kuwasiri msafara wa mateka wa Ahlulbait (a.s) katika mji wa Madina

Maoni katika picha
Baadhi ya riwaya zinaonyesha kuwa katika siku kama hizi mwaka wa 61h, msafara wa mateka wa Ahlulbait (a.s) uliwasiri katika mji wa Madina, wakiwa wanatembea kidogo kidogo hakuna wanacho wahia, huku macho ya wanawake wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) yakiwa yamejaa machozi kwa kuwalilia ndugu zao waliouawa, na wanakumbuka manyanyaso waliyofanyiwa, mji wa Madina ulikua umejaa huzuni kufuatia kifo cha mama wa waislamu Ummu Salama Mke wa Mtume (s.a.w.w), aliyefariki baada ya kifo cha Imamu Hussein (a.s) kwa muda wa mwezi mmoja.

Imamu Zainul-Aabidina (a.s) alipofika karibu na mji wa Madina, alisimama na kuweka kambi, halafu akamuambia Bishru bun Hadhlam: “Ewe Bishru, Mwenyezi Mungu amrehemu baba yako, alikua mshairi, je unaweza kusoma shairi?”. Akasema: Ndio ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Akasema: “Nenda katika mji wa Madina na usome shairi la kumuomboleza Abu Abdillah”.

Bishru akaenda hadi Madina, alipofika katika jumba ya Mtume, akapandisha sauti yake iliyojaa kilio, akasema:

Enyi watu wa Madina hamna kukaa, Hussein ameuawa lieni.

Muili wake uko Karbala umetupwa, na kichwa juu ya mkuki kinazungushwa.

Watu wakakusanyika kwa wingi katika nyumba ya Mtume, huku wanalia na kutaka habari zaidi kutoka kwa Bishru, walimzunguka na kumuuliza, kuna habari gani?

Akawaambia: Ali bun Hussein pamoja na shangazi yake na dada zake wamekuja, kaniagiza nije kukuambieni sehemu walipo, watu wote wakaanza kulia, wakaondoka haraka kwenda kupokea familia ya Mtume (s.a.w.w), vilio vilienea kila mahala, sauti zikawa juu, wanaume walimzunguka Zainul-Aabidina wakiwa wanalia, siku hiyo ikawa sawa na siku aliyokufa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).

Imamu Zainul-Aabidina akasoma hutuba kali, akaeleza yaliyoitokea familia ya Mtume, mauaji, mateso na kutekwa, mambo ambayo hata milima inaweza kutetemeka, Swa’aswa’ah akamuomba samahani Imamu kwa kushindwa kwenda kumsaidia na kumnusuru Hussein (a.s), Imamu akakubali udhuru wake na akamrehemu baba yake.

Kisha Imamu pamoja na shangazi yake na dada zake wakaondoka kuelekea Madina wakiwa wamezungukwa na kundi kubwa la watu wanaolia kwa sauti, wakaenda hadi kwenye nyumba ya Mtume, walipo fika bibi Zainabu akashika mlango wa nyumba, akaanza kumueleza babu yake Mtume (s.a.w.w) na kumpa pole kwa kufiwa na mjukuu wake, akasema: “Ewe babu yangu, mimi nakupa pole kwa kufiwa na kaka yangu Hussein”.

Wanawake wa familia ya Mtume wakaomboleza kifo cha bwana wa mashahidi, wakavaa nguo nyeusi, wakaendelea kuomboleza kwa majonzi makubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: