Kuangalia historia ya maisha ya Sukaina mtoto wa Imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi tano Rabiul-Awwal mwaka wa (117h) alifariki Sukaina mtoto wa Imamu Hussein (a.s), jina lake ni (Amina) na inasemekana ni (Amiina) alipewa jina la (Sukaina) kutokana na utulivu wake, mama yake anaitwa Rabaab mtoto wa Imriu-Alqais. Amekua mashuhuri kwa jina la (Sukaina) kwa sababu ya utulivu wake na unyenyekevu.

Riwaya zinaonyesha kuwa alizaliwa (a.s) mwaka wa arubaini na saba hijiriyya, wakati wa kifo cha baba yake Imamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala, alikua na umri wa miaka kumi na nne, aliyoishi chini ya uangalizi wa baba yake bwana wa mashahidi (a.s), kulelewa na maasumu kuna athari kubwa katika kumjenga kwenye kielimu, kidini, kitabia pamoja na athari ya mazingira ya familia yenye zaidi ya maasumu mmoja na watukufu wengine, alikua na kiwango cha juu cha elimu na maadili mema, alishuhudia mauaji wa Karbala, aliona kwa macho yake yaliyotokea Karbala, alimuona baba yake na kaka zake wakiwa wameuawa juu ya jangwa, alitekwa na kuishi maisha ya mateka, aliona madhila waliyofanyiwa familia ya Mtume (s.a.w.w) katika mji wa Kufa na Sham, alionyesha msimamo wake mbele ya wanawake na watoto, alimjibu Ubaidullahi bun Ziyaad na Yazidi bun Muawiya, kisha alirudi na kaka yake Imamu Zainul-Aabidina (a.s) na mateka wengine katika mji wa Madina.

Baada ya vita ya Twafu Sukaina (a.s) alikuwa katika uangalizi wa Imamu Sajjaad (a.s), aliishi Maisha yaliyojaa elimu na adabu, zama zake zilijaa elimu, akili, adabu, uchamungu, alipamba vikao vya wanawake wa Madina kwa elimu, adabu na uchamungu wake, alikua mfasaha.

Alifariki (a.s) siku kama ya leo katika mji wa Madina na akazikwa kwenye makaburi ya Baqii, amani iwe juu yake siku aliyozaliwa na siku aliyokwenda kwa Mola wake akiwa na kumbukumbu ya kuhuzunisha ya Ashura na siku atakayo fufuliwa akiwa mbele ya vichwa vya mashahidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: