Kurejea swala za jamaa katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) Adhuhuri ya leo siku ya Jumanne mwezi 5 Rabiul-Awwal mwaka 1443h sawa na tarehe 12 Oktoba 2021m imeswaliwa swala ya Adhuhuri kwa jamaa, nayo ni swala ya kwanza kuswaliwa kwa jamaa baada ya kusimama kwa zaidi ya mwaka kutokana na janga la virusi vya Korona.

Swala hiyo imeongozwa na Mheshimiwa Shekh Swalahu Karbalai rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, sambamba na kuchukua tahadhari za kiafya na umbali kati ya mtu na mtu.

Watumishi wa kitengo cha haram tukufu wameandaa sehemu maalum za kuswali wanaume na wanawake, na kuweka alama zinazo onyesha sehemu ya kusimama mtu anayeswali, pamoja na kuweka vizuwizi vinavyo tenganisha sehemu za kuswalia, na kuweka watumishi wanaosimamia umbali wanaotakiwa kusimama baina yao wakati wa swala.

Swala ya jamaa huswaliwa kila simu, waumini wanatakiwa kuswali swala za faradhi kwa jamaa, amma swala ya Ijumaa yenyewe lazima iswaliwe kwa jamaa na bado imesimama hadi litakapotolewa tamko.

Kumbuka kuwa swala za jamaa zilisimama kuswaliwa ndani ya haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu, tangu lilipotokea janga la maambukizi ya virusi vya Korona mwaka jana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: