Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Taasisi ya kimataifa ya Waarith ya kutibu uvimbe ni mradi muhimu wa kibinaadamu

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar amesema kuwa, hakika mradi wa taasisi ya kimataifa ya Waarith ya kutibu uvimbe ni mradi muhimu wa kibinaadamu, unatoa huduma nzuri kwa wananchi wa Iraq, unaonyesha namna Atabatu Husseiniyya na kiongozi wake mkuu wa kisheria wanavyo lijali taifa hili lenye uchache wa vituo na taasisi za kutoa huduma hiyo kwa watu wenye matatizo hayo.

Ameyasema hayo wakati ujumbe maalum kutoka Atabatu Abbasiyya ukiongozwa na yeye pamoja na wajumbe kadhaa wa kamati kuu na marais wa vitengo, ulipotembelea kituo hicho kutoa pongezi kwa watumishi wa taasisi hiyo na viongozi wa Atabatu Husseiniyya tukufu chini ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai, sambamba na kuangalia huduma zinazo tolewa kwa wagonjwa waliolazwa hapo.

Akaongeza kuwa: “Yafaa kujivunia taasisi hii, inauwezo mkubwa na vifaa vya kisasa, pamoja na kuwa na majengo mazuri na watumishi wenye kujituma na uaminifu mkubwa katika kuhudumia wagonjwa, hakika viongozi wa taasisi hii wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kituo hiki kinakua cha kwanza kwa kutoa huduma bora inayokubalika kimataifa, bila shaka kituo hiki kimepunguza usumbufu kwa wagonjwa, tunawashukuru na kuwaomba wahudumu wa taasisi hii wafanikiwe katika kazi yao”.

Ugeni umetembelea sehemu nyingi na kuangalia vitengo vyote vya hospitali, wamesikiliza maelezo ya huduma zinazo tolewa na kuangalia vifaa tiba vya kisasa walivyonavyo, katika matembezi hayo waliongozana na kiongozi wa kamati ya afya na elimu ya udaktari katika Atabatu Husseiniyya tukufu, Dokta Sattaar Saidiy ambaye ameonyesha furaha kubwa kwa kutembelewa na ugeni huo, akasema kuwa hiyo ni ishara ya ushirikiano uliopo kati ya Ataba mbili tukufu, pamoja na kuwa ziara hiyo itaongeza hamasa ya kufanya vizuri zaidi kwa wahudumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: