Chuo kikuu Alkafeel kinapokea wanafunzi na kimetangaza kuanza mwaka mpya wa masomo

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuanza mwaka mpya wa masomo (2021 – 2022), kimeanza kupokea wanafunzi wa vitivo vyote, mwaka huu unatarajiwa kuwa wa pekee na kuendeleza mafanikio ya chuo.

Rais wa chuo cha Alkafeel Dokta Nuris Muhammad Shahidi Dahani amewapongeza wanafunzi, walimu na watumishi kwa kuanza mwaka mpya wa masomo, amewahimiza kuongeza juhudi ili waweze kufanikiwa katika kutumikia jamii na kuendeleza elimu katika taifa letu kipenzi.

Akasisitiza kuwa: “Chuo kimefanya kazi kubwa kuhakikisha kinatimiza mahitaji yote ya lazima kielimu na kuandaa mazingira mazuri ya usomaji, sambamba na kutekeleza masharti ya kujikinga na maambukizi kwa ajili ya kuhakikisha usalama kwa wote”. Akasema: “Uongozi wa chuo na wakuu wa vitivo wamejitahidi kutatua changamoto zote”.

Naye Dokta Nawaal Aaid Almayali makamo rais wa chuo ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Chuo kupitia vitivo vyake vyote kimekamilisha mapema maandalizi ya kupokea wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo, chini ya maelekezo ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, tunatarajia uwe mwaka wa mafanikio kielimu”.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Alkafeel katika mji mtukufu wa Najafu, kinafanya kila kiwezolo kuleta maendeleo ya kielimu, kitamaduni, kimalezi na kitafiti hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: