Maahadi ya Qur’ani tawi la Bagdad inafanya nadwa kwa anuani isemayo (Mtume na sheria ya kuvumiliana)

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Bagdad chini ya Atabatu Abbasiyya, imefanya nadwa ya Qur’ani yenye anuani isemayo: (Mtume na sheria ya kuvumiliana), chini ya uhadhiri wa Shekh Qassim Baidhwani na kuhudhuriwa na kundi la waumini.

Nadwa imefanywa katika wilaya ya Husseiniyya kaskazini mashariki ya mji wa Bagdad, imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ahmadi Aamiriy, kisha mtafiti akawasilisha mada yake iliyohusu sheria za Mwenyezi Mungu zilizo fundishwa na Mtume (s.a.w.w), zinazo saidia kuweka maisha mazuri na maelewano baina ya watu, pamoja na kuwafundisha itikadi, ibada, tabia njema, kazi na taratibu za maisha.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Bagdad hufanya nadwa za Qur’ani kila mwezi, kwa lengo la kufundisha elimu ya vizito viwili vitukufu.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani ni moja ya kituo muhimu cha kufundisha Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inasaidia kutengeneza jamii yenye ujuzi wa Qur’ani katika nyanja zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: