Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatoa semina kwa watumishi wapya wa shule za Al-Ameed.
Rais wa kitengo hicho Dokta Ahmadi Kaabi amesema: “Kila mwaka huwa tunakua na semina elekezi kwa watumishi wapya, kwa lengo la kuwajengea uwezo kielimu na kimalezi, ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa mafanikio”.
Akaongeza kuwa: “Semina hizi hufanywa chini ya malengo ya kitengo ya kuleta mageuzi ya malezi, kwa kuandaa walimu na kuwapa mbinu za lazima katika kujiandaa na mwaka mpya wa masomo”.
Akaendelea kusema: “Semina imekua na vitu vingi, zikiwemo mada tofauti kuhusu mbinu za ufundishaji zinazo weza kutumiwa na mwalimu katika chumba cha darasa, ambazo humsaidia mwanafunzi kuonyesha uwezo na kipaji chake”.
Kumbuka kuwa kitengo cha malezi na elimu hufanya semina, warsha na mashindano ya kielimu, kwa lengo la kuongeza uwezo wa walimu.