Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza msiba na jengo lake limevishwa vazi la msiba

Maoni katika picha
Mazingira ya huzuni yametanda kwenye korido na kuta za Atabatu Abbasiyya tukufu, kama ishara ya kuomboleza kifo cha walii wa Mwenyezi Mungu na mteule wake Imamu wa kumi na moja baba wa Imamu wa zama, Imamu Hassan bun Ali Azzakiiy Askariy (a.s), ambaye tarehe aliyokufa inasadifu Ijumaa ya kesho mwezi nane Rabiul-Awwal.

Muonekano wa huzuni ni sehemu ya kumpa pole Imamu wa zama (a.f) kwa kufiwa na baba yake (a.s), na kuungana na Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao na wafuasi wao katika msiba huu mkubwa, unaoliza na kuhuzunisha roho, uliotokea mwaka wa (260h) dunia ikamkosa Imamu Askariy (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu kama kawaida yake kwenye kila tukio la kidini linalohusu kumbukumbu ya kifo cha Ahlulbait (a.s) huandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huo.

Kumbuka kuwa waumini miongoni mwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia wanaomboleza msiba huu na kumpa pole Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.f), kwa kufiwa na baba yake Imamu Hassan Askariy (a.s), aliyeuawa na kiumbe dhalimu zaidi, Mu’tamad Abbasi alimpa sumu kali iliyosambaa katika muili wa Imamu (a.s), na kumuuguza kwa simu kadhaa huku akifanya subira na kumtegemea Mwenyezi Mungu, hatimae akafa akiwa na umri wa miaka ishirini na nane, katika siku ya mwezi nane Rabiul-Awwal mwaka (260h).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: