Shule za Al-Ameed zipo tayali kupokea wanafunzi wake

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuwa shule za Al-Ameed zipo tayali kupokea wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo (2021 – 2022m), baada ya kukabidhiwa rasmi majengo ya shule hizo na kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kilicho simamia ujenzi wa majengo hayo.

Majengo ya shule yapo katika barabara ya (Karbala – Huru) kwenye kiwanja chenye ukubwa wa (2m45,000), kuna jumla ya shule tano, kila shule moja inaukubwa wa mita (6000), inauwezo wa kupokea idadi kubwa ya wanafunzi, kwani kila jengo linaghorofa tatu, kuna shule za awali mbili, kila moja inaukubwa wa mita (900) na kuna kumbi mbili za michezo, kila moja inaukubwa wa mita (900), zinatumika kwa michezo na mapumziko, zinatumiwa na wanafunzi wa shule pamoja na watoto wa chekechea, sambamba na majengo hayo ya shule kuna kituo cha utamaduni pia, ambacho ni alama kuu sehemu hiyo, kuna maghorofa matano yenye ukubwa wa mita za mraba elfu (15), pamoja na sehemu za bustani.

Rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Ahmadi Swabihi Kaabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika mradi huu ni muendelezo wa miradi mingi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya ujenzi wa shule za (msingi, sekondari, vyuo na vituo vya utamaduni), katika kuchangia kutoa huduma ya elimu kwa njia za kisasa bila kuathiriwa na tamaduni za kigeni ambazo zimeanza kuingia katika jamii ya raia wa Iraq, tunachangia kuwapa watoto elimu bora yenye maadini ya kiislamu chini ya mfumo maalum”.

Akaongeza kuwa: “Majengo hayo yanachangia kuweka mazingira mazuri ya kusoma, nayo ni hatua nzuri katika sekta ya elimu hapa Iraq hususan Karbala, vifaa vyote vya lazima katika ufundishaji na usomaji vimewekwa kwenye majengo hayo, kuna mradi mwingine utakamilika hivi karibuni unaohusu wanafunzi”.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi (Ddiyaau Majidi Swaaigh) amesisitiza kuwa “Mradi huu ukosawa na miradi ya kimataifa, bali unazidi miradi ya kimataifa katika baadhi ya mambo kwenye sekta ya usanifu na utekelezaji”.

Akasema: “Katika utekelezaji wa mradi huu tumejikita katika mambo mawili makuu upande wa masomo, nayo ni mazingira ya shule na mazingira ya darasani, nao ni moja ya miradi inayopewa umuhimu mkubwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na umuhimu wake katika kuboresha sekta ya elimu hapa Karbala, nao ni miongoni mwa miradi yenye kiwango cha juu, kutokana na usasa wa mradi huo”.

Akamaliza kwa kusema: “Mradi wote kwa ujumla umejengwa kisasa, unakidhi mahitaji ya wazazi na watoto, majengo yanabustani za kupumzika na sehemu kubwa za kucheza wanafunzi, pamoja na maabara, sehemu za kulia chakula na uwanja mkubwa kwa kila shule, aidha kunakumbi za ndani kubwa za michezo pamoja na mengine ambayo hutakiwa na mwanafunzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: