Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil inatafuta ushirikiano na vitivo viwili

Maoni katika picha
Ugeni kutoka maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, umetembelea vyuo vikuu kadhaa katika mkoa wa Baabil, kwa lengo la kujenga ushirikiano kati yao.

Wametembelea kitivo cha malezi ya msingi katika chuo kikuu cha Baabil na kitivo cha Imamu Alkaadhim (a.s), ugeni huo umeongea na wakuu wa vitivo hivyo kuhusu uboreshaji wa somo la Qur’ani hapa mkoani, na kushirikiana pamoja na vitivo hivyo katika harakati mbalimbali, wakapongeza kazi kubwa inayofanywa na wakuu wa vitivo hivyo.

Nao wakuu wa vitivo hivyo wameshukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Baabil, kutokana na kuzi kubwa wanayofanya kwenye sekta ya Qur’ani hapa mkoani, sambamba na juhudi ya kusambaza mafundisho ya vizito viwili katika korido za vyuo.

Tambua kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil, hufanya harakati mbalimbali za Qur’ani tukufu, zikiwemo semina endelevu za Qur’ani katika mkoa huo.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya kituo muhimu cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kazi yake kubwa ni kusambaza elimu ya Qur’ani, na kusaidia kutengeneza jamii yenye uwelewa wa Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: