Kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s)

Maoni katika picha
Siku ya mwezi nane Rabiul-Awwal ni kumbukumbu ya kifo cha Maasumu wa kumi na tatu baada ya Mtume (s.a.w.w), na Imamu wa kumi na moja katika maimamu wa Ahlulbait (a.s) na mzazi wa Imamu msubiriwa Hassan bun Ali Azzakiy Al-Askariy (a.s), iliyekufa mwaka wa 260 hijiriyya kwa sumu aliyopewa na watawala wa Abbasiyya wa kipindi hicho, kupitia Mu’tamadi Abbasiyya.

Imamu Hassan Askariy (a.s) alichukua majukumu ya Uimamu baada ya kifo cha baba yake Imamu Ali Alhaadi (a.s) mwaka wa (253h), utawala wa Abbasiyya haukumuacha salama Imamu Hassan Askariy (a.s), walimuweka chini ya ulinzi mkali, na walifuatilia harakati zake zote.

Katika kipindi cha uimamu wake kilikua ni kipindi cha watawala wafuatao: Mu’tazu, Muhtada na Mu’tamad katika watawala wa bani Abbasi, watawala wote watatu walimnyanyasa na kumtesa Imamu (a.s), watawala hao walikua watu waovu jambo lililosababishwa wachukiwe na watu.

Imamu alipata aina balimbali za mateso kutoka kwa Mu’tamad, pia aliwekewa ulinzi mkali, walizuwia kila mtu aliyetaka kuwasiliana nae, sababu ya watawala wa bani Abbasi kufanya hivyo ilikua ni husda yao kwa Imamu Askariy (a.s) na hofu yao kwa Imamu Mahadi (a.f), ambaye walijua wazi kuwa atazaliwa na Imamu Askariy (a.s).

Baada ya mateso yote waliyofanya kwa Imamu (a.s) Mu’tamad akampa sumu iliyouguza muili wa Imamu (a.s) kwa siku kadhaa hadi akafariki akiwa na umri wa miaka ishirini na nane, akafa kishahidi mwaka (260h).

Imamu Hassan Askariy (a.s) alimuacha mwanae Hujjat Almuntadharu Almahadi (a.s), mwanae wa pekee kwa ajili ya kusimamisha utawala wa uadilifu na kuokoa wanyonge na kueneza uislamu kila sehemu ya dunia, kama alivyo ahidi babu yake Mtume (s.a.w.w) kwenye hadithi nyingi zilizopo katika makundi yote ya kiislamu.

Alizikwa pamoja na baba yake Imamu Haadi (a.s) katika nyumba yake huko (Samaraa) sehemu ambapo makaburi yao yapo hadi leo, na hutembelewa na wapenzi wa Ahlulbait na kutabaruku pamoja na kutawasul kwa Mwenyezi Mungu mtukufu kwa utukufu wao.

Kaburi zao zimekua amani kwa watu wa pande mbili, Shekh Tusi amepokea riwaya isemayo: (Hakika kaburi langu katika mji wa Samaraa ni amani ya nchi kutokana na maafa, Imamu Askariy (a.s) alisema kwa watu wa pande mbili).

Majlisi wa kwanza anasema: Watu wa pande mbili wanaokusudiwa ni Shia na Sunni, baraka zake (a.s) humuendea Rafiki na adui, kama lilivyo kaburi la babu yake Mussa Alkaadim (a.s) ni amani kwa watu wa Bagdad.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: