Kuhudumia mazuwaru wa Askariyyaini: Vimefunguliwa vituo vya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefungua vituo vya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu katika sura fupi na nyeradi za swala kwa mazuwaru wanaokwenda katika malalo ya maimamu wawili Askariyyaini (a.s).

Vituo vya ufundishaji wa Qur’ani vinaendeshwa kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya kwenye barabara zinazo elekea katika malalo takatifu, vinafundisha Qur’ani tukufu hususan surat Faat-ha na Tauhiid pamoja na nyeradi wa swala, kwasababu hayo ndio mambo muhimu katika kusihi kwa swala.

Hali kadhalika vituo hivyo vinajukumu la kujibu maswali ya mazuwaru na kutoa ufafanuzi wa mambo tofauti ya kisheria, na kugawa folda zenye nyaraka zinazohusu ziara na mambo tofauti ya Qur’ani, vituo hivyo vimewekwa kwenye barabara zinazotumiwa na mazuwaru wengi, huduma hiyo imekua ikitolewa na Maahadi ya Qur’ani kwa miaka mingi, ni sehemu ya muendelezo wa mafanikio ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), na ziara ya kiongozi wa waumini katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).

Vituo vimepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru, hasa tabaka la vijana ambao bado hawajamaliza masomo, na wazee ambao hawawezi kusoma vizuri, nao ndio walengwa zaidi wa mradi huu, hakika kusihi kwa swala kunategemea usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: