Watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wameshiriki kwenye ratiba ya kuhudumia waombolezaji katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) huko Samaraa, wamefanya kazi pega kwa pega na ndugu zao watumishi wa Atabatu Askariyya.
Kwa mujibu wa maelezo aliyotoa kwenye mtandao wa Alkafeel Sayyid Naim Aboudi Hassan kutoka kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu: “Ushiriki huu umetokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Ataba tukufu, tumeshiriki katika Nyanja tofauti, kama tulivyokua tukishiriki siku za nyuma kwenye ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu katika malalo hizi mbili takatifu Askariyyain (a.s), chini ya ratiba iliyopangwa kwa ajili ya kazi hiyo, kwa lengo la kutoa huduma bora, aidha ni sehemu ya kusaidia kazi nzuri inayofanywa na Atabatu Askariyya na Ataba zingine.
Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa huduma tulizo toa ni kugawa maji safi ya kunywa kutoka kituo cha (RO) kwa mazuwaru na mawakibu za kutoa huduma zilizopo kwenye barabara zote zinazo elekea katika malalo takatifu chini ya utaratibu maalum, aidha tumetoa magari ya usafi kwa ajili ya kusaidia kubeba taka, sambamba na hayo watumishi wetu wamegawa barafu kwa mawakibu za kutoa huduma kupitia gari maalum za kusambaza barafu, ambazo zinachukua barafu katika kiwanda cha barafu cha Atabatu Abbasiyya na kuzileta Samaraa”.
Akaendelea kusema: “Hali kadhalika makundi mbalimbali ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya yameshiriki kutoa huduma tofauti katika Atabatu Askariyya takatifu, kazi inaendelea kwa zaidi ya siku tatu, na kilele chake ilikua siku aliyofariki, na wataendelea kutoa huduma hadi mazuwaru watakapoisha”.
Kitengo cha usafiri cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimeshiriki kubeba mazuwaru kutoka sehemu za vituo vya nje hadi karibu na haram, pamoja na kubeba mazuwaru wakazi wa Karbala hadi Samaraa na kuwarudisha.
Kiwanda cha barafu cha Atabatu Abbasiyya kimegawa kiasi kikubwa cha barafu kwa mawakibu za kutoa huduma.
Kumbuka kuwa ushirikiano unaofanywa na Atabatu Abbasiyya sio jambo geni, unatokana na kuhisi majukumu ya kusaidia kufanikisha ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, na kunufaika na uzowefu walionao wa mambo tofauti, wanafanya kazi chini ya kauli mbiu isemayo (kuhudumia zaairu ni fahari yetu) katika kila eneo linapotajwa jina la watu wa nyumba ya Mtume (a.s).