Mwezi tisa Rabiul-Awwal kumbukumbu ya kuvishwa taji la Uimamu Baqiyyatu-Llahi

Maoni katika picha
Wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) mashariki na magharibi ya dunia, katika siku kama ya leo mwezi tisa Rabiul-Awwal huadhimisha kuvishwa taji la uongozi Imamu Mahadi msubiriwa (a.f), nakuchukua rasmi mamlaka ya Uimamu baada ya kifo cha baba yake Imamu Hassan Askariy (a.s) mwaka wa (260h).

Imamu Mahadi (a.f) alichukua jukumu la Uimamu akiwa na miaka mitano, hivyo ni Imamu aliyechukua madaraka akiwa na umri mdogo zaidi, jambo hilo sio geni katika historia ya Mitume, Manabii na Maimamu wa Ahlulbait (a.s).

Baadhi ya Mitume walipewa mamlaka wakiwa bado wadogo, kama vile Nabii Issa na Yahya (a.s), kwa mujibu wa ushahidi wa Qur’ani tukufu, walipewa mamlaka wakiwa na miaka nane, na babu yake Imamu Haadi alipewa Uimamu akiwa na miaka nane, na Imamu Jawaad (a.s) wakati anapewa Uimamu alikua na miaka saba au tisa.

Shekh Abdurahmaani Jaami Alhanafii katika kitabu cha Mir-Aatu Asraar anapo muelezea Imamu Mahadi (a.s) anasema: “Wakati wa kifo cha baba yake Imamu Hassan Askariy alikua na umri wa miaka mitano, akakalia kiti cha Uimamu, kama jinsi Mwenyezi Mungu alivyo mpa hekima na utukufu Yahya mtoto wa Zakariya akiwa mdogo, na akampandisha daraja kubwa Issa mwana wa Maryam wakati wa utoto wake, hali kadhalika katika miaka ya utoto Mwenyezi Mungu alimfanya kuwa Imamu, mambo yasiyo yakawaida yaliyo dhihiri kwake sio machache, tutosheke na muhtasari huu..”.

Jukumu lake la kwanza baada ya kupata Uimamu lilikua na kumswalia baba yake Imamu Hassan (a.s) mdani ya nyumba yake, kabla ya kutoa muili wake rasmi kwa ajili ya kuuswalia, utawala wa kipindi kile ulifanya njama iliyofeli na kuthibitisha Uimamu wake, kwani kanuni inasema Imamu maasumu haswaliwi ispokua na Imamu maasumu kama yeye, katika siku hiyo Imamu Mahadi (a.s) alitoweka machoni kwa watu baada ya kumswalia baba yake, na hapo ikaanza ghaiba ndogo iliyodumu kwa muda wa mika sabini.

Tukio hili hufurahisha na kuadhimishwa na wapenzi wa Ahlulbait (a.s), kwa sababu ni siku ya kwanza ya Uimamu wa muokozi wa binaadamu, na Imamu wa mwisho, humuomba Mwenyezi Mungu mtukufu amdhihirishe haraka Imamu Mahadi msubiriwa (a.s), aje kujaza dunia haki na uadilifu baada ya kujaa dhulma na uovu, kama alivyo bashiri babu yake Muhammad (s.a.w.w) katika hadithi mutawatira zilizo andikwa na vitabu vya waislamu wote Sunni na Shia.

Katika siku kama ya leo inapendekezwa kutoa sadaka na kugawa chakula, na kusaidia wanafamilia, imepokewa kuwa atakaetoa katika siku hii Mwenyezi Mungu atamsamehe dhambi zake, pia ni vizuri kuvaa nguo mpya na kumshukuru Mwenyezi Mungu na kufanya idaba, ni siku ya kuondoa matatizo na huzuni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: