Zaidi ya mazuwau elfu 23 wamefanyiwa ziara ya Imamu Askariy (a.s) kwa niaba katika malalo yake takatifu

Maoni katika picha
Kundi la masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya ziara ya Imamu Hassan Askariy (a.s), katika kumbukumbu ya kifo chake kwenye malalo yake takatifu huko Samaraa kwa niaba ya watu (23,687) kutoka ndani na nje ya Iraq, waliojisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba uliopo katika mtandao wa kimataifa Alkafeel, toguti rasmi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na maelfu mengine ya watu waliojisajili kwenye mitandao ya mawasiliano ya kijamii iliyochini yake.

Kiongozi wa idara ya Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Sayyid Hashim Shami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumepata utukufu wa kuwafanyia ziara watu waliojisajili kwenye ukurasa huo, ambapo siku baada ya siku idadi ya watu wanaojisajili inaongezeka, tumefanya ziara kwa niaba ya kila aliyeshindwa kuja kufanya ziara, hali kadhalika hatuja wasahau wapenzi wote na wafuasi wa Maimamu wa Ahlilbait (a.s) wa dunia nzima, tumewaombea dua wapate afya na amani kwa baraka za muadhimishwa huyu mtukufu”.

Akaongeza kuwa: “Tulikuwepo katika malalo ya Maimamu wawili watakatifu Al-Askariyyain (a.s) katika mji wa Samaraa, tumefanya ziara zaidi ya mara moja, ikiwemo ziara maalum na ziarat Jaamia na swala ya ziara, pamoja na dua na kusoma baadhi za aya na kuelekeza thawabu zake kwa watu wote walio jisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba”.

Kumbuka kuwa dirisha la ziara kwa niaba linamuitikio mkubwa kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel, ni njia muhimu ya mawasiliano inayo onganisha mazuwaru na wapenzi pamoja na malalo za Maimamu (a.s), watu walio jisajili kwenye ukurasa huo ni zaidi ya milioni nne (4,000,000) kutoka ndani na nje ya Iraq, ni ukurasa wa kwanza kufunguliwa kwa ajili ya kufanya ziara kwa niaba ya kila aliyeshindwa kuja kufanya ziara na kutabaruku yeye mwenyewe kutokana na umbali au kwa sababu nyingine yeyote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: