(Wapiga picha) tunaangazia vipaji vya wanawake wapiga picha

Maoni katika picha
Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya imefungua mtandao wa mawasiliano na kuupa jina la (Wapiga picha), kwa lengo la kubaini vipaji vya wanawake katika upigaji wa picha, pamoja na kuwashajihisha katika kazi ya upigaji wa picha ambayo imekua na umuhimu mkubwa katika maisha ya sasa.

Mkuu wa maktaba bibi Asmaa Al-Abaadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kufungua mtandao huo ni sehemu ya mkakati wa maktaba wa kukuza vipaji vya wanawake na kuviendeleza, tumetenga ukurasa maalum kwenye toghuti yake, wa kuonyesha picha walizo piga”.

Akaongeza kuwa: “Sehemu ya picha inaonyesha utamaduni na turathi za kiislamu, kwa kupiga picha majengo ya malalo matakatifu na mazaru tukufu, pamoja na maeneo yanayobeba ujumbe wa ubinaadamu katika utamaduni wa kiislamu kwenye matukio ya kidini na mengineyo”.

Akafafanua kuwa: “Kuna kamati maalum yenye jukumu la kuchuja picha na kuchagua zinazofaa kuwekwa kwenye mtandao, kutakua na zawadi watakazo pewa watakao piga picha nzuri kila baada ya muda fulani”.

Kwa maelezo zaidi au kushiriki kutuma picha, fungua link ifuatayo: https://alkafeel.net/women_library/#/art/945
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: